Na. Chrispin Kalinga - Ludewa
Wizara ya afya kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti Malaria (NMCP) kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI inatekeleza afua mbalimbali za kudhibiti ugojwa wa malaria ikiwa na lengo la kutokomeza ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030 kwa kuhakikisha wananchi wote wanatumia vyandarua vilivyowekewa dawa ya muda mrefu ya kuuwa mbu.
Miongoni mwa afua zinazo tumika katika kupambana na kudhiti ugonjwa wa malaria ni pamoja na Ugawaji wa vyandarua kwa akinamama wajawazito hudhurio la kwanza la kliniki,
Watoto wa umri wa miezi tisa wanao stahili kupata chanjo ya Surua Rubella
Wazee kuanzia miaka 60 nakuendelea waliotibiwa OPD,
Wateja wa CTC wanaohudhuria vituoni
Watoto umri chini ya miaka mitano, waliolazwa na Kutibiwa Malaria kali,
akina mama wajawazito wanapewa kinga tiba kuanzia wiki la 14 anapohudhuria kiliniki pamoja
Kufanya usafi wa mazingira ili mbu asipate mazalia.
Halmashauri ya wilaya ya Ludewa yenye Kata 26 na vijiji 77 inaendelea na mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria.
Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa kushirikiana na Wizara ya afya kupitia Bohari ya dawa(MSD)
imekuwa ikigawa vyandarua kwa makundi mbalimbali ikiwemo wanafunzi wa shule ya msingi , ambapo Novemba 08, 2023 zoezi la ugawaji vyandarua lilizunduliwa Wilayani Ludewa Kwa kuanza kugawa kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi darasa la sita Zaidi ya wanafunzi 26,333 katika shule 117 ikiwa shule 113 ni za serikali na 4 ni binafsi.
Ludewa - Njombe
Sanduku la Barua: 19
Simu: 026-2790120
Simu ya Rununu:
Barua Pepe: ded@ludewadc.go.tz
Copyright ©2022Ludewadc . All rights reserved.